Jumapili 24 Agosti 2025 - 22:49
Mmoja wa walimu wa Hawza ya  Najaf Ashraf afariki dunia

Hawzah/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Muhammad Ali Bahr al-Ulum, mmoja wa walimu wa Hawza ya Najaf Ashraf, ameaga dunia

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Muhammad Ali Bahr al-Ulum, mmoja wa walimu wa Hawza ya Najaf Ashraf, alasiri ya jana Jumamosi, baada ya kupatwa na kiharusi cha ghafla wakati wa safari kwa ndege, aliaga dunia.

Vyanzo vilivyo karibu na Al-Forat News vimeripoti kwamba marehemu alipata tatizo la ghafla la kiafya akiwa ndani ya ndege, na jitihada za kumrejesha hazikufua dafu, jambo lililopelekea kifo chake cha haraka.

Familia ya Aal Bahr al-Ulum imetoa rambirambi kwa kuondokewa na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Muhammad Ali Bahr al-Ulum, mwalimu wa Hawza ya kielimu Najaf, na wameeleza masikitiko makubwa kwa kumpoteza mwanachuoni huyu mashuhuri.

Kwa kuzingatia msiba huu mchungu, familia ya Aal Bahr al-Ulum kuanzia saa 4 asubuhi siku ya Jumapili tarehe 29 Safar 1447 Hijria Qamariyya hadi wakati wa kuwasili kwa mwili wa mwanachuoni huyu Najaf Ashraf, watapokea salamu za rambirambi na ta’zia katika ukumbi wa mikutano wa familia.

Marehemu alikuwa miongoni mwa walimu wa Hawza ya Najaf Ashraf na mtoto wa Ayatullah Sayyid Muhammad Bahr al-Ulum (quddisa sirruh).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha